Lugha Nyingine
Hungary yatoa wito wa hatua za kimataifa za kuzuia kuongezeka kwa mgogoro wa Gaza

Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary Peter Szijjarto (Kulia) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Israel Katz mjini Budapest, Hungary, Juni 17, 2024. (Picha na Attila Volgyi/Xinhua)
BUDAPEST - Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary Peter Szijjarto ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzuia mgogoro wa Gaza kuzidi kuongezeka na kuwa vita kati ya nchi kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Israel, Israel Katz.
"Mashariki ya Kati kimsingi ndiyo inaamua hali ya usalama duniani, na iwapo kuna mgogoro au janga la kiusalama katika Mashariki ya Kati, daima inaleta tishio kwa usalama wa kimataifa. Mgogoro wa sasa wa Gaza unaweza kuwa tishio kubwa la usalama duniani," Szijjarto amesema, huku akiongeza kuwa kama nchi nyingine itahusika katika mgogoro huo, inaweza kugeuka kirahisi kuwa vita vikali ambavyo vinaenea nje ya mipaka ya nchi inayofuata.
Israel imekuwa ikifanya mashambulizi makubwa dhidi ya Kundi la Hamas ili kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya kushtukiza ya kundi hilo katika miji ya kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana, ambapo Waisrael takriban 1,200 waliuawa na zaidi ya 200 kuchukuliwa mateka.
Mashambulizi hayo ya miezi minane ya Israel yamesababisha Wapalestina zaidi ya 37,000 kuuawa na wengine 85,000 kujeruhiwa, kwa mujibu wa mamlaka ya afya ya Gaza.
Mashambulizi hayo ya Israel pia yamegeuza sehemu kubwa za eneo hilo kuwa magofu na kusababisha janga kubwa la kibinadamu katika eneo hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary Peter Szijjarto (Kulia) akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Israel Katz mjini Budapest, Hungary, Juni 17, 2024. (Picha na Attila Volgyi/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



