

Lugha Nyingine
Kenya yasema iko njiani kukabiliana na kuenea kwa jangwa
(CRI Online) Juni 18, 2024
Kenya imeadhimisha Siku ya Kupambana na Hali ya Kuenea kwa Jangwa na Ukame Duniani, wakati ikiendelea na kazi ya kukabiliana na misukusuko hiyo, na kufanikiwa kupanua eneo la misitu hadi zaidi ya asilimia kumi ya ardhi yake.
Waziri wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu wa Kenya Soipan Tuya, aliyeongoza sherehe zilizofanyika Laikipia katika Bonde la Ufa nchini Kenya, amesema ukubwa wa eneo la miti nchini Kenya umefikia asilimia 12.3 ya ardhi yake.
Waziri Tuya amesema hii ni hatua kubwa katika kukabiliana na hali ya kuenea kwa jangwa, kuvia kwa ardhi na ukame, amekuwa akizunguka nchi nzima kuendesha kampeni ya upandaji miti, na kwamba mkakati huo wa kihistoria umehimiza kurejesha mfumo ikolojia nchini Kenya.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma