

Lugha Nyingine
China, EU zafanya mazungumzo kuhusu mazingira na tabianchi
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Maros Sefcovic mjini Brussels, Ubelgiji, Juni 18, 2024. (Xinhua/ Shen Hong)
BRUSSELS - Mazungumzo ya tano ya ngazi ya juu kuhusu mazingira na tabianchi kati ya China na Umoja wa Ulaya (EU) yaliyoongozwa na Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang na Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Maros Sefcovic yamefanyika siku ya Jumanne mjini Brussels, huku pande zote mbili zikikubaliana kuzidisha ushirikiano katika sekta ya kijani.
Ding, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema katika miaka ya hivi karibuni, Rais Xi Jinping wa China na viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekuwa na mikutano ya mara kwa mara na kufikia makubaliano mengi kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya katika mageuzi ya kijani.
Ding amebainisha kuwa China imekuwa ikitambua mara kwa mara nafasi muhimu ya Ulaya katika Dunia yenye ncha nyingi na inauchukulia Umoja wa Ulaya kama kipaumbele muhimu cha mambo ya diplomasia ya China na pia kama mshirika muhimu wa kufikia ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
"Tunahitaji kufanya kazi pamoja ili kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa China na Umoja wa Ulaya, kusukuma mbele zaidi kuelekea ushirikiano wenye mafanikio mengi zaidi katika mageuzi ya kijani, na kuimarisha kasi ya uhusiano thabiti na mzuri kati ya China na Umoja wa Ulaya," Ding amesema.
Amesema kuwa China imetekeleza kithabiti mkakati wake wa kitaifa wa kushughulikia mabadiliko ya tabianchi, na kupata mafanyikio makubwa katika maendeleo ya kijani na yenye kutoa kaboni chache. Amebainisha kuwa China imekuwa mshiriki, mchangiaji, na kuongoza katika ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia duniani.
Ding amesisitiza kuwa magari yanayotumia umeme ni bidhaa muhimu ya kubadilisha muundo wa nishati ya kijani, na mpango wa EU wa kuweka ushuru wa ziada kwa magari yanayotumia umeme yanayoagizwa kutoka China ni "namna fulani ya kujihami kibiashara."
"Hatua hiyo haisaidii kubadilisha muundo wa nishati ya kijani ya EU na inaweza kudhoofisha ushirikiano wa kimataifa juu ya mabadiliko ya tabianchi," amesema.
Kwa upande wake Sefcovic amesema China ina ushawishi mkubwa katika masuala ya kimataifa, na kudumisha uhusiano mzuri na China kuna umuhimu mkubwa kwa EU. Amepongeza hatua kali za China na mafanikio makubwa katika kuhimiza maendeleo ya kijani na yenye kutoa kaboni chache.
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Maros Sefcovic mjini Brussels, Ubelgiji, Juni 18, 2024. (Xinhua/ Shen Hong)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma