Waziri Mkuu wa China Li Qiang awasili Malaysia kwa ziara rasmi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 19, 2024

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur nchini Malaysia, Juni 18, 2024. (Xinhua/Li Tao)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur nchini Malaysia, Juni 18, 2024. (Xinhua/Li Tao)

KUALA LUMPUR - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amewasili Kuala Lumpur, Malaysia siku ya Jumanne kwa ziara rasmi nchini humo, ikiwa ni kituo cha tatu na cha mwisho cha ziara yake ya siku nane ambayo imemfikisha New Zealand na Australia ambapo alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili 50 miaka iliyopita, uhusiano huo umeendelezwa vizuri, na hali ya kuaminiana kimkakati imeimarishwa.

Pia, mawasiliano ya kitamaduni na kati ya watu yamekuwa ya karibu zaidi, na ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja umezaa matunda mazuri, ambayo yameleta manufaa halisi kwa watu wa nchi hizo mbili na kutoa mchango katika amani na maendeleo ya kikanda, amesema.

Waziri Mkuu Li amebainisha kuwa mwaka jana, Rais Xi Jinping wa China na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim walifikia makubaliano muhimu ya kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na Malaysia yenye mustakabali wa pamoja, na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya China na Malaysia.

China ingependa kushirikiana na Malaysia, kuchukua maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili kama sehemu mpya ya kuanzia ili kuimarisha zaidi kuunganisha mikakati ya maendeleo, kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, kuimarisha mawasiliano ya utamaduni na kujifunza kutoka kwa kila mmoja, na kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya China na Malaysia yenye mustakabali wa pamoja, ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa amani, utulivu, maendeleo na ustawi katika kanda na duniani kote, Waziri Mkuu Li amesema.

Waziri Mkuu Li amewasili Kuala Lumpur baada ya kuhitimisha ziara rasmi nchini Australia na kufanya Mkutano wa tisa wa Mwaka wa Viongozi wa China na Australia na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese.

Akiwa nchini Malaysia, Waziri Mkuu Li atakuwa na mazungumzo na Mfalme wa Malaysia Sultan Ibrahim Sultan Iskandar na Waziri Mkuu Anwar Ibrahim, na kuhudhuria hafla ya kuadhimisha miaka hiyo 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur nchini Malaysia, Juni 18, 2024. (Xinhua/Li Tao)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur nchini Malaysia, Juni 18, 2024. (Xinhua/Li Tao)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha