Lugha Nyingine
Kiongozi Mkuu wa DPRK akutana na Rais wa Russia
(Picha inatoka Xinhua)
Shirika la Habari la Taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) limeripoti kuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo Bw. Kim Jong Un amempokea Rais wa Russia Vladimir Putin aliyewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pyongyang kwa ziara ya kiserikali nchini humo.
Bw. Kim Jong Un ameeleza kufurahia kukutana tena na Rais Putin baada ya siku 270 tangu wakutane kwenye kituo cha kurusha vyombo kwenda anga ya juu cha Vostochny nchini Russia mwezi Septemba mwaka jana.
Rais Putin pia amemshukuru kiongozi huyu kumkaribisha katika uwanja wa ndege, na baada ya hapo, viongozi hao wamefanya mazungumzo ya kirafiki kwenye Jumba la Wageni la Taifa la Kumsusan.
Shirika hilo pia limesema ziara hiyo ya Rais Putin ina umuhimu mkubwa katika kuhimiza maendeleo ya kimkakati ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika siku zijazo.

people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma