

Lugha Nyingine
Rais wa Rwanda azishutumu nchi za Magharibi kwa undumilakuwili wa demokrasia kabla ya uchaguzi
(CRI Online) Juni 19, 2024
Rais Paul Kagame wa Rwanda amezishutumu nchi za Magharibi kwa undumilakuwili wa demokrasia, kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika mwezi ujao nchini humo.
Bw. Kagame, ambaye amekuwa Rais wa Rwanda tangu mwaka 2000 amesema hayo alipokuwa akijibu swali kuhusu wakosoaji waliomshutumu kung'ang'ania madaraka.
Rais Kagame amesema demokrasia inahusu uhuru wa maamuzi, na kwamba hajui mahali popote ambapo demokrasia imefanikiwa wakati kanuni na maadili yake vyote vinaamriwa kutoka nje.
Kauli hiyo ya Kagame imetolewa siku kadhaa baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo kutoa idhini kwa yeye na wagombea wengine wawili kushiriki kwenye uchaguzi wa rais utakaofanyika mwezi ujao.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma