

Lugha Nyingine
Kampuni za China kushiriki katika maonyesho makubwa ya biashara ya Tanzania
(CRI Online) Juni 19, 2024
Kaimu mkurugenzi wa ukuzaji wa biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw. Tito Nombo amesema kundi la kampuni za China litashiriki kwenye maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam (DITF) yatakayofanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13.
Bw. Nombo amesema nchi nyingine 10 pia zinatarajiwa kushiriki katika maonesho hayo ya mwaka huu yenye kauli mbiu ya "Tanzania: Kituo Chako Bora Kwa Biashara na Uwekezaji."
Bw. Nombo amesema maonyesho hayo yanalenga kutangaza bidhaa na huduma, kusaidia waonyeshaji kufikia masoko mapya na kutafuta fursa mpya.
Mfadhili mkuu wa maonyesho hayo ya biashara ni Kampuni ya mambo ya ugavi ya China iliyoko Afrika Mashariki, inayojihusisha na biashara ya kimataifa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma