

Lugha Nyingine
Kenya yasema bwawa lililojengwa na kampuni ya China litakuwa na manufaa mengi
(CRI Online) Juni 19, 2024
Waziri wa Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji kwa Kenya Bw. Zacharia Njeru amesema Bwawa la Thwake lililojengwa na kampuni ya China kwenye kaunti ya Makueni, linakaribia kukamilika, na kuanza kutumika kwake baadaye mwaka huu kutafungua njia ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi nchini Kenya.
Bw. Njeru amesema bwawa hilo linatarajiwa kuimarisha usambazaji wa maji, umwagiliaji, na uzalishaji wa umeme katika maeneo yenye ukame mashariki mwa Kenya.
Bwawa hilo limejengwa na kampuni ya Gezhouba ya China na kugharamiwa kwa pamoja na serikali ya Kenya na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), pia litasaidia kutatua suala la ukosefu wa usalama wa chakula na maji kwa kaya na mifugo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma