

Lugha Nyingine
China, Malaysia zinaleta uhusiano wa pande mbili katika mwanzo mpya - Waziri Mkuu wa China
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihutubia tafrija ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Malaysia na Mwaka wa Urafiki wa China na Malaysia pamoja na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Juni 19, 2024. (Xinhua/Li Tao)
KUALA LUMPUR - China na Malaysia zimeleta uhusiano wa pande mbili katika mwanzo mpya, na zina matarajio ya pamoja ya kuusongesha mbele kwa vizazi vijavyo, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema siku ya Jumatano wakati akitoa hotuba yake kuu wakati alipohudhuria tafrija ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Malaysia na Mwaka wa Urafiki wa China na Malaysia pamoja na Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim.
Li amesema, kama Rais Xi Jinping wa China alivyosema, China na Malaysia ni majirani wenye urafiki wa miaka 100, marafiki waliounganishwa na moyo, na wenzi wa ushirikiano wa kunufaishana.
"Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, nchi hizo mbili zimeweka dhamira kwa mikakati ya kujiamuliwa, ushirikiano wa kunufaishana, kusaidiana na mawasiliano ya utamaduni," Li amesema, huku akiongeza kuwa maendeleo ya uhusiano huu yanatoa uzoefu mwingi muhimu na hamasa, ambavyo ni mali ya thamani kwa pande zote mbili.
Alisema kuwa mwaka huu ni Mwaka wa Urafiki wa China na Malaysia, "urafiki" ni neno lenye uzito mkubwa, ambao ni thamani sana leo.
Amesema kuwa hii ni dunia ambayo inakosa amani na utulivu, lakini kamwe kusiwe na migongano na migogoro; dunia inayokosa busara na unyenyekevu, lakini kamwe kusiwe na vitendo vya kiholela na vya kikatili; dunia inayokosa huruma, lakini kamwe kusiwe na ubinafsi; na dunia inayokosa uwazi na ushirikiano, lakini kamwe kusiwe na kuweka vizuzi na mapambano.
"Dunia inapaswa kuweka mkazo zaidi katika ushirikiano wa kunufaishana, na kuachana kabisa na fikra na vitendo vya mmoja kupata na wengine kukosa," Li amesema, huku akiongeza kuwa Dunia inapaswa pia kujaribu zaidi kusimama katika nafasi za wengine, na kushikilia kanuni ya "usiwafanyie wengine yale usiyotaka wengine wakufanyie."
Li amesema kuwa shughuli za Mwaka wa Urafiki wa China na Malaysia hazikupangwa kwa lengo tu la kukuza uhusiano wa pande mbili, bali pia kuhamasisha moyo wa urafiki, na kutoa wito na kushikamana zaidi kutoka pande zote za Dunia ili kuungana mikono na kuvuka kwenda mustakabali bora wa pamoja wa siku za baadaye.
Kwenye hotuba yake, Anwar amesema urafiki kati ya Malaysia na China una historia ndefu.
Tangu viongozi wa nchi hizo mbili wafanye uamuzi wa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia miaka 50 iliyopita, uhusiano kati ya Malaysia na China umekuwa na maendeleo makubwa, na kuleta manufaa makubwa kwa watu wa pande hizo mbili, amesema.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim wakipeana zawadi za ukumbusho kabla ya tafrija ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Malaysia na Mwaka wa Urafiki wa China na Malaysia mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Juni 19. 2024. (Xinhua/Rao Aimin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma