UNDP, Benki ya Dunia zatoa wito kwa Botswana kuruhusu sekta binafsi kuongoza uchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 20, 2024

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Botswana, Balazs Horvath akihutubia Mkutano wa 2 wa Kila Mwaka ESG (Mazingira, Uendelevu na Utawala) wa Botswana na Baraza la Uendelevu wa Mambo ya Fedha mjini Gaborone, Botswana, Juni 19, 2024. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

GABORONE – Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Benki ya Dunia zimetoa wito kwa Botswana kuruhusu sekta binafsi kuchukua nafasi kubwa katika shughuli za kiuchumi nchini humo kwa ajili ya kutumiza ukuaji na maendeleo ya haraka.

Wakizungumza kwenye Mkutano wa 2 wa Kila Mwaka ESG (Mazingira, Uendelevu na Utawala) wa Botswana na Baraza la Uendelevu wa Mambo ya Fedha mjini Gaborone, Botswana siku ya Jumatano, washirika hao wawili wa maendeleo wamesema Botswana inahitaji kushirikiana zaidi na sekta ya kibinafsi ili kutatua changamoto za uendelevu za nchi hiyo.

Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini humo, Balazs Horvath amesema mamlaka za serikali zinatakiwa kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya malengo ya kijamii na yale ya kibiashara, akitaja kuwa kanuni na sera zinapaswa kutengenezwa ili kuhakikisha kuwa sekta ya kibinafsi inafuata miundo ya kupata faida bila kukanyaga mahitaji ya kijamii.

"Kuwa na nafasi kubwa sana ya mashirika ya serikali ni ghali sana na kuyafanya makampuni hayo kuendelea," amesema Horvath, akitoa wito kwa sekta ya kibinafsi kuruhusiwa kuchukua nafasi kubwa katika shughuli za kiuchumi.

Akitoa maoni hayo hayo, Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini humo Liang Wang amesema Botswana inahitaji kuhama kutoka uchumi wa umma kwenda uchumi unaoongozwa na sekta ya kibinafsi, na ESG ndio kiini cha mpito.

"Kuna haja kwa serikali kutounda mashirika mengi ya serikali bali kuruhusu sekta ya kibinafsi kuchukua uongozi," amesema Wang, huku akipendekeza kuwa sekta ya kibinafsi inatakiwa kuongeza thamani wakati serikali inalinda dhidi ya ushindani usio na usawa.

Pia amesisitiza kuwa kutoa ajira kutakuwa jukumu la sekta ya kibinafsi.

Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Botswana Liang Wang akihutubia Mkutano wa 2 wa Kila Mwaka ESG (Mazingira, Uendelevu na Utawala) wa Botswana na Baraza la Uendelevu wa Mambo ya Fedha mjini Gaborone, Botswana, Juni 19, 2024. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha