Kampuni ya China yaanza uzalishaji wa chuma kizito nchini Zimbabwe

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 24, 2024

Mfanyakazi akiwa na pilika nyingi za kazi kwenye Kampuni ya Dinson Iron and Steel (DISCO) huko Manhize, Jimbo la Midlands, Zimbabwe, Juni 20, 2024. (Picha na Shaun Jusa/Xinhua)

Mfanyakazi akiwa na pilika nyingi za kazi kwenye Kampuni ya Dinson Iron and Steel (DISCO) huko Manhize, Jimbo la Midlands, Zimbabwe, Juni 20, 2024. (Picha na Shaun Jusa/Xinhua)

MANHIZE - Kampuni ya Dinson Iron and Steel (DISCO), ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni binafsi ya Kundi la Kampuni za Tsingshan Holding katika Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, imeanza uzalishaji wa chuma kizito huko Manhize, mji ulioko Jimbo la Midlands nchini Zimbabwe, ikimaanisha kufikiwa kwa hatua kubwa za ufufukaji wa viwanda vya chuma nchini humo.

"Kwa kweli hili ni tukio la furaha sana kuona hatua ya kwanza ya uzalishaji wa chuma kutoka Manhize," amesema Waziri wa Migodi na Maendeleo ya Madini wa Zimbabwe Winston Chitando katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua baada ya kutembelea kiwanda cha DISCO siku ya Alhamisi.

Chuma hicho kizito, ambacho pia kinajulikana kuwa ni chuma ghafi, ni bidhaa ya moja kwa moja ya tanuri ya mlipuko na kutoa zao la chuma, chuma cha pua, au chuma safi sana kinaposafishwa.

Uzalishaji wa chuma hicho kizito, ambao ulianza wiki iliyopita, unaweka mazingira tayari ya uzalishaji wa billet ya chuma, ambao unatarajiwa kuanza mwezi ujao.

Chitando amesema DISCO inatarajiwa kuzalisha tani 600,000 za chuma cha kaboni katika kipindi cha kwanza cha ujenzi wa mradi huo, na kuongezeka hadi milioni 1.2, kisha milioni 3.2 na hatimaye tani milioni 5 kwa mwaka katika kipindi cha mwisho.

Amesema maendeleo hayo ni ushahidi wa ushirikiano kati ya China na Zimbabwe. "Zimbabwe na China zimekuwa na uhusiano wa kisiasa wa muda mrefu, na hapa sasa tuna uhusiano wa kiuchumi unaoimarisha uhusiano huo wa kisiasa."

Wilfred Motsi, mkurugenzi wa mradi wa Kundi la Kampuni za Dinson, amesema maendeleo hayo yanaonesha hatua kubwa ya ukuaji wa viwanda nchini Zimbabwe.

"Tunarejea katika siku zetu za utukufu wakati Zimbabwe ilipojulikana ni moja ya vituo vya viwanda kusini mwa Afrika kwa sababu ya kufunguliwa kwa sekta ya chuma," Motsi amesema. "Hatuzungumzii tena kuwa viwanda vya chuma vimekufa Zimbabwe. Ndiyo, baadhi ya wadau walikuwepo, lakini (wao) walikuwa wanazalisha kwa kiwango kidogo, lakini kuingia kwetu kunamaanisha kuwa tumefufua viwanda vya chuma nchini Zimbabwe. " 

Wafanyakazi wakiwa na pilika nyingi za kazi katika Kampuni ya Dinson Iron and Steel (DISCO) huko Manhize, Jimbo la Midlands, Zimbabwe, Juni 20, 2024. (Picha na Shaun Jusa/Xinhua)

Wafanyakazi wakiwa na pilika nyingi za kazi katika Kampuni ya Dinson Iron and Steel (DISCO) huko Manhize, Jimbo la Midlands, Zimbabwe, Juni 20, 2024. (Picha na Shaun Jusa/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha