Watu 200 wajeruhiwa, 100 wakamatwa nchini Kenya kufuatia maandamano kupinga muswada wa sheria ya kodi

(CRI Online) Juni 24, 2024

Watu 200 wamejeruhiwa na wengine 100 wamekamatwa nchini Kenya katika maandamano ya kundi la wanaopinga muswada wa sheria unaoanzisha na kuongeza kodi mbalimbali nchini humo.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa mtu mmoja ambaye hakujulikana jina amefariki dunia katika Kituo cha Afya cha Blisa baada ya kupigwa risasi kwenye maandamano hayo, huku mtu mwingine anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 29 amefariki wakati akipatiwa matibabu katika kituo hicho siku ya Alhamisi wiki iliyopita.

Waandamanaji hao wanapinga bajeti ya mwaka huu iliyosomwa hivi karibuni ambayo imelenga kuongeza kiasi cha Sh bilioni 2.7 cha mapatao ya serikali kupitia miswada ya sheria yenye kuanzisha na kuongeza kodi mbalimbali.

Waandamanaji hao wanadai watunga sheria wapige kura kupinga muswada huo wa sheria ya matumizi ya serikali wenye kuongeza na kuanzisha kodi mbalimbali ambayo wanasema itakuwa mzigo kwa watumishi na wajasiriamali nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha