Wake wa marais wa China na Poland watembelea Kituo cha Taifa cha Sanaa za Maonesho mjini Beijing

(CRI Online) Juni 25, 2024

Mke wa Rais wa China Peng Liyuan na mke wa Rais wa Poland Agata Kornhauser-Duda Jumatatu alasiri walitembelea Kituo cha Taifa cha Sanaa za Maonyesho kilichopo mjini Beijing.

Bibi Peng Liyuan amesema, China na Poland zote zina historia ndefu na urithi mkubwa wa kiutamaduni, katika miaka ya hivi karibuni mabadilishano ya kiutamaduni kati ya pande hizo mbili yameongezeka siku hadi siku. Anaamini kuwa maelewano na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili utaimarika zaidi kutokana na kupanuka kwa mabadilishano hayo ya kiutamaduni.

Bibi Peng alimwalika Bibi Agata kutazama kwa pamoja maonesho ya muziki wa jadi wa China, opera ya Beijing, muziki wa piano wa kichina na kipoland na kwaya ya nyimbo za kichina na za kigeni.

Bibi Agata amemshukuru Bibi Peng kwa mapokezi mazuri, na kusema amevutiwa na utamaduni mkubwa wa jadi wa kichina, na anatarajia kuwa pande hizo mbili zitaimarisha zaidi ushirikiano na mabadilishano, ili kuzidisha urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha