

Lugha Nyingine
Kuwezesha wanawake wa Kenya kwavunja vizuizi katika ujenzi wa Bwawa la Thwake
Victoria Mutweleli, mwendesha eskaveta wa Kampuni ya China Gezhouba, akifanya kazi kwenye mradi wa Bwawa la Thwake huko Makueni, Kenya, Juni 17, 2024. (Xinhua/Lin Jing)
NAIROBI - Akikabiliana na joto kali la alasiri, Victoria Mutweleli alikuwa akitumia gia za eskaveta kubwa juu ya kingo za Bwawa la Thwake, ambalo liko mpaka wa Kaunti ya Makueni, kusini-mashariki mwa Kenya.
Mama huyo wa makamo wa watoto wawili alikuwa akitabasamu wakati eskaveta hiyo ikichota mawe ya ukubwa wa kati na kuyaweka juu ya kingo kwa ajili ya kusagwa, ikiashiria kukamilika kwa awamu ya kwanza ya bwawa hilo la matumizi mbalimbali la Thwake, ambalo ujenzi wake chini ya Kampuni ya Gezhouba ya China (CGGC) ulianza Machi 2018.
Akiwa ni mhitimu wa uendeshaji wa mitambo mikubwa katika chuo cha kiwango cha kati, Mutweleli awali alifanya kazi katika Reli ya Kisasa ya Mombasa-Nairobi (SGR) wakati wa ujenzi wake, ambapo aliendesha eskaveta, mashine za kusaga na na kuviringisha vitu.
Mwaka 2019, Mutweleli alipokea ofa ya kazi kutoka CGGC ya kuwa mwendeshaji eskaveta, ikimpa nafasi ya kuendeleza ujuzi wake katika kazi za uhandisi wa ujenzi, nyanja inayotawaliwa na wanaume.
"Tangu nianze kufanya kazi katika mradi wa Bwawa la Thwake, naweza kusema kwamba nimepata ujuzi na uzoefu wa kuendesha mashine nzito," amesema Mutweleli kwenye mahojiano ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China, Xinhua.
Yeye ni miongoni mwa wafanyakazi wa kike ambao wamepingana na dhana potofu na kutoa utaalam wao kwenye ujenzi wa bwawa hilo ambalo linatarajiwa kuimarisha usambazaji wa maji, umwagiliaji na uzalishaji wa umeme katika kaunti kame za kusini mashariki mwa Kenya.
Bwawa la Thwake ambalo linafadhiliwa na serikali ya Kenya na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ni mradi mkuu wa Dira ya 2030 ya nchi hiyo. Unatekelezwa kwa awamu nne, zikijumuisha uwekaji wa kingo ambao uko karibu kukamilika, miundombinu ya usambazaji maji, uzalishaji wa umeme kwa nishati ya maji na umwagiliaji.
Zachariah Njeru, Waziri anayeshughulikia Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji wa Kenya, amesema kwenye ziara ya hivi karibuni ya ukaguzi wa bwawa hilo kwamba litatoa maji yaliyotibiwa yanayofikia mita za ujazo karibu 150,000 kila siku kwa watu milioni 1.3 katika eneo la chini la mashariki.
"Ninaendesha zaidi ya mashine moja, ninaendesha mashine za kunyanyua na kusogeza vitu vizito” amesema Mukami, ambaye alijiunga na mradi huo wa bwawa mapema mwaka huu lakini tangu Mwaka 2009 amekuwa akiendesha mashine nzito nchini Kenya na ng'ambo.
Picha iliyopigwa Juni 18, 2024 ikionyesha eneo la ujenzi wa mradi wa Bwawa la Thwake huko Makueni, Kenya, Juni 17, 2024. (Kundi la Kampuni za China Gezhouba)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma