

Lugha Nyingine
China kufanya mkutano wa kuadhimisha miaka 70 tangu kutangazwa kwa Kanuni Tano za Kuishi pamoja kwa Amani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Bi. Mao Ning amesema kuwa China itafanya Mkutano wa Kuadhimisha Miaka 70 tangu kutangazwa kwa Kanuni Tano za Kuishi pamoja kwa Amani siku ya Ijumaa mjini Beijing.
Miongo saba iliyopita, Waziri Mkuu wa wakati huo wa China Zhou Enlai alitangaza kanuni hizo kikamilifu kwa mara ya kwanza, "kuheshimiana mamlaka na ukamilifu wa ardhi, kutokandamizana, kutoingiliana mambo ya ndani, usawa na kunufaishana, na kuishi pamoja kwa amani".
Ameongeza kuwa Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani zimekubaliwa na kutambuliwa na nchi zote duniani na zimekuwa jadi ya kawaida inayoongoza uhusiano wa kisasa wa kimataifa.
Amesema, shughuli za shamrashamra za maadhimisho hayo zitajumuisha kufanyika kwa mkutano mkuu wa maadhimisho, tafrija rasmi ya chakula cha mchana na majukwaa yatakayofanyika sambamba. Amesema, Rais Xi Jinping wa China atahudhuria mkutano mkuu wa maadhimisho na kutoa hotuba, na Waziri Mkuu Li Qiang ataongoza mkutano huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma