Mkuu wa Jimbo la Gauteng asema serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Afrika Kusini haitabadilisha sera

(CRI Online) Juni 27, 2024

Mkuu wa Jimbo la Gauteng nchini Afrika Kusini Panyaza Lesufi amesema kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya sera kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ya Afrika Kusini (GNU).

Lesufi kutoka chama cha African National Congress (ANC) ameyasema hayo mjini Johannesburg kwenye mkutano wa kuhimiza ushirikiano wa kibiashara kati ya Beijing na Afrika Kusini. Ambapo Baraza la Kuendeleza Biashara ya Kimataifa la China (CCPIT) Tawi la Beijing limeongoza ujumbe wa jumuiya ya wafanyabiashara kwenda Johannesburg kutafuta fursa za biashara na ushirikiano na wenzao wa Afrika Kusini.

Lesufi ameongeza kuwa alipotembelea China, alifurahishwa na usalama wake ambao angependa kuona hali hiyo ikijitokeza nchini Afrika Kusini.

Afrika Kusini ipo kwenye mchakato wa kuijenga Johannesburg kuwa jiji la kisasa, amesema Lesufi, huku akisisitiza ushirikiano na China utasaidia nchi hiyo kufikia lengo hilo.

Amesema, Afrika Kusini inaitazama China katika kuboresha maendeleo ya miundombinu, treni za mwendo kasi na kukabiliana na uhaba wa nishati.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha