

Lugha Nyingine
Mashirika ya kibinadamu ya UN na washirika wao wapanua opresheni za msaada huko Darfur na Khartoum nchini Sudan
Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (UN) Jumatano yalisema wao pamoja na washirika wao wanajitahidi kupanua operesheni za msaada huko Darfur na Khartoum nchini Sudan, haswa katika El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini.
Shirika la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa (OCHA) limesema hali ya El Fasher na sehemu zake za karibu zinaleta wasiwasi mkubwa.
Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), watoto zaidi ya 400 wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa vibaya kwenye mapambano ya hivi karibuni.
Limesema, muendelezo wa matumizi ya silaha za mlipuko kwenye maeneo yenye watu wengi umeleta hatari zaidi kwa raia na watu wanaotoa msaada.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeripoti kuwa linasambaza msaada wa dharura wa chakula na lishe kwa watu zaidi ya 135,000 katika jimbo la Al-Jazirah nchini humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma