China yapinga Marekani na nchi nyingine za Magharibi kuhamisha lawama juu ya mgogoro wa Ukraine

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 28, 2024

BEIJING - Wu Qian, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China ameelezea upinzani mkali dhidi ya Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi kwa kuhamisha lawama juu ya mgogoro wa Ukraine.

Wu ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi alipokuwa akijibu swali kuhusu Taarifa ya hivi karibuni ya Viongozi wa G7.

Wu amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa asilimia zaidi ya 60 ya vitu vinavyohusu silaha na bidhaa zenye matumizi ya aina mbili zinazoagizwa nje ya nchi na Russia zinatoka Marekani na nchi nyingine za Magharibi.

Mwenendo huu wa kudumisha biashara na Russia huku ukiingilia na kudhoofisha ushirikiano wa kawaida kati ya China na Russia ni wa kinafiki kupindukia, amesema.

"Badala ya kutafakari juu ya mchango wao katika mgogoro wa Ukraine, Marekani na nchi nyingine za Magharibi zimekuwa zikihamishia lawama kwa China mara kwa mara, jambo ambalo tunalipinga vikali," msemaji huyo amesema.

Wu amesema, China imekuwa ikifanya mawasiliano ya kawaida ya kiuchumi na kibiashara na nchi zote, ikiwa ni pamoja na Russia, kwa msingi wa usawa na kunufaishana, lakini haitoi silaha za mashambulizi kwa upande wowote katika mgogoro huo, huku ikidhibiti vikali uuzaji nje wa bidhaa zenye matumizi ya aina mbili.

China siku zote imesimama upande wa amani na upande sahihi wa historia. Inapinga kithabiti shutuma zisizo na msingi, na itaendelea kutoa mchango wa kiujenzi katika suluhu ya kisiasa kwa mgogoro wa Ukraine, amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha