

Lugha Nyingine
EU na Ukraine zatia saini makubaliano ya usalama
Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel (Kulia) na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakiwasili kwa ajili ya mkutano wa kilele wa Baraza la Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji, Juni 27, 2024. (Xinhua/Zhao Dingzhe)
BRUSSELS - Umoja wa Ulaya (EU) na Ukraine zimetia saini makubaliano ya usalama kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ulaya mjini Brussels siku ya Alhamisi ambapo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alihudhuria mkutano huo na kutia saini makubaliano hayo ya usalama pamoja na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel na Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, EU na nchi wanachama wake hadi sasa zimetoa euro karibu bilioni 108 (kama dola bilioni 115.6 za Kimarekani) za msaada kwa Ukraine.
"EU ina nia ya kuendelea kuipatia Ukraine na watu wake misaada yote inayohitajika wa kisiasa, kifedha, kiuchumi, kibinadamu, kijeshi na kidiplomasia kwa muda mrefu kama itakavyochukua na kwa nguvu kama itakavyohitajika," nyaraka za makubaliano hayo zimeeleza.
EU pia imekubali kutumia mapato yasiyo ya kawaida yanayotokana na mali za Russia zilizozuiliwa barani humo ili kuisaidia Ukraine, kwa mujibu wa makubaliano hayo.
Makubaliano hayo pia yamesisitiza kuwa Ukraine inapaswa kuendeleza mageuzi yake kuendana na njia yake ya kujiunga na Umoja wa Ulaya, na kuimarisha hatua za uwazi na uwajibikaji kuhusu misaada iliopokea.
Von der Leyen ameahidi kwenye mtandao wa kijamii wa X kuendelea kutoa silaha, mafunzo ya kijeshi na misaada ambayo Ukraine inahitaji. "Hii inasisitiza: tuna mpango wa muda mrefu," ameongeza.
Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel (Kulia) na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakiwasili kwa ajili ya mkutano wa kilele wa Baraza la Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji, Juni 27, 2024. (Xinhua/Zhao Dingzhe)
Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel (Kulia) na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakizungumza na waandishi wa habari kabla ya mkutano wa kilele wa Baraza la Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji, Juni 27, 2024. (Xinhua/Zhao Dingzhe)
Washiriki wakipiga picha ya kundi kabla ya mkutano wa kilele wa Baraza la Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji, Juni 27, 2024. (Xinhua/Zhao Dingzhe)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma