Maandamano yaendelea nchini Kenya licha ya kuondolewa kwa mswada wa kuongeza ushuru

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 28, 2024

NAIROBI - Maandamano yameendelea nchini Kenya siku ya Alhamisi, licha ya uamuzi wa Rais William Ruto ya kuacha mapendekezo ya kuongeza ushuru na ahadi yake ya kuweka hatua za kubana matumizi ambapo mamia ya watu wameingia katika mitaa ya miji mbalimbali nchini Kenya, ingawa idadi yao ilikuwa ndogo ikilinganishwa na mapema wiki hii.

Wamekaidi ombi la Rais Ruto na naibu wake, Rigathi Gachagua, ambao Jumatano walikuwa wamewataka kusitisha maandamano na kufanya mazungumzo na serikali. Waandamanaji hao wamesema walikuwa wakiandamana kukumbuka wenzao waliofariki au kujeruhiwa katika maandamano ya awali.

Jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, wanajeshi na maafisa wa polisi wa kutuliza ghasia walikuwa wamezagaa mitaa mingi. Katika baadhi ya mitaa, waandamanaji hao waliwasha mishumaa na kuiweka kando ya maua ya waridi, wakiimba nyimbo za mazishi. Pia waliandika majina ya waliodaiwa kuuawa kwenye maandamano hayo kwenye karatasi za manila, wakiorodhesha majina 18, wengi wao wakiwa wenye umri wa miaka 20.

Watu takriban sita wamepoteza maisha na wengine 214 kujeruhiwa kwenye maandamano ya Jumanne, kwa mujibu wa taarifa ya serikali. Wengi wa waliofariki wameuawa bungeni wakati polisi walipofyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wamevunja taratibu za usalama na kuvamia jengo la bunge.

Rais Ruto ameelezea kusikitishwa na vifo hivyo na kusema kuwa serikali itaunda mfumo wa kuhakikisha uwajibikaji.

Waandamanaji hao baadaye walikabiliana na polisi siku ya Alhamisi katikati mwa jiji la Nairobi, ambao walikuwa wakijaribu kuwatawanya kwa kutumia gesi ya kutoa machozi. Waandamanaji kadhaa walikamatwa na kuchukuliwa katika magari ya polisi.

Ukaguzi wa usalama ulikuwa umeimarishwa katika barabara kuu zote zinazoelekea eneo kuu la biashara la Nairobi, lakini maofisa usalama hawakabiliana na watu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha