Mkutano wa mafanikio ya Mahojianano ya pamoja ya kujenga“Ukanda Mmoja,Njia Moja” kwa kiwango cha juu ya People’s Daily na Vyombo vya Habari vya Kazakhstan wafanyika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 01, 2024

Baraza la Juu la Bunge la Kazakhstan, Sarybaev Galiaskar Tulendinovich na Alisher Satvaldiyev, Naibu mhariri mkuu wa People’s Daily Xu Lijing, Meneja Mkuu wa Kundi la Magazeti ya Kazakh ambalo gazeti la “Kazakhstan Pravda” liko chini yake Tihan Kamzabekuray, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Habari la Kimataifa la "Kazinform" Askar Zaldinov, Konsela wa Ubalozi wa China nchini Kazakhstan Liu Hua na wengineo walihudhuria kwenye mkutano huo.

Washiriki wa mkutano huo walisema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, China na Kazakhstan zimeendeleza kwa kina na halisi ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kwa kiwango cha juu na kupata mafanikio mengi. Wanatumai vyombo vya habari vya nchi hizi mbili vinaweza kuonesha umuhimu wao zaidi ulio kama daraja na kiungo, kufanya ushirikiano kwa njia mpya, kusimulia vizuri hadithi za Njia ya Hariri, na kusukuma mbele maendeleo na ustawi kwa pamoja.

Mkutano huo uliandaliwa na Gazeti la People's Daily na kusaidiwa na Shirika la Watafiti wa China ya Kazakhstan. Takriban wajumbe 40 kutoka sekta za siasa, taaluma na vyombo vya habari vya China na Kazakhstan walihudhuria. Mkutano huo pia ulifanya hafla ya kutangazwa kwa mabango ya ng’ambo ya kusoma magazeti ya kielektroniki ya People's Daily, hafla ya kutolewa kwa filamu ya rikodi ya “Ushindi wa Pamoja” ya People's Daily Online, na hafla ya kukusanya kazi za utangazaji wa kimataifa wa "Silk Road Award".

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha