

Lugha Nyingine
Rais wa Afrika Kusini Atangaza Orodha ya Baraza lake jipya la Mawaziri
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia taifa kwa njia ya televisheni mjini Pretoria, Afrika Kusini, Juni 30, 2024. (Ofisi ya Mawasiliano na Habari wa Serikali ya Afrika Kusini/Xinhua)
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini alitangaza orodha ya baraza lake jipya la mawaziri Jumapili, linalojumuisha mawaziri kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa vinavyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU).
Tangazo hilo lilitolewa zaidi ya wiki moja baada ya kuapishwa kwa Ramaphosa Juni 19 kwa muhula wake wa pili wa rais. Lakini hakupata viti vingi kwenye uchaguzi, na kulazimisha chama chake, African National Congress, kugawanya madaraka kwa mara ya kwanza katika miongo mitatu iliyopita.
Hii ilisababisha kuundwa kwa GNU vikiwemo vyama 10 vya upinzani kama vile Democratic Alliance (DA), Inkatha Freedom Party, Pan Africanist Congress ya Azania, na vinginevyo.
Katika hotuba yake ya kitaifa, Ramaphosa alitangaza kwamba uchumi na utulivu wa serikali zitakuwa jambo linalofuatiliwa zaidi kwa baraza jipya la mawaziri.
"Serikali mpya itaweka kipaumbele ukuaji wa uchumi wa haraka, shirikishi na endelevu na kujenga jamii yenye haki zaidi kwa kushughulikia umaskini na ukosefu wa usawa," alisema rais.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia taifa kwa njia ya televisheni mjini Pretoria, Afrika Kusini, Juni 30, 2024. (Ofisi ya Mawasiliano na Habari wa Serikali ya Afrika Kusini/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma