

Lugha Nyingine
Umoja wa Afrika wasema hautaitelekeza Somalia
(CRI Online) Julai 02, 2024
Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kimekabidhi kituo cha kijeshi cha Abdalle Birolle kwa Jeshi la Taifa la Somalia (SNA), kuashiria uhamisho wa kituo cha nne cha kijeshi kama sehemu ya awamu ya tatu ya uondoaji wa askari wa ATMIS nchini Somalia.
Kwenye taarifa yake iliyotolewa mjini Mogadishu, ATMIS imesema kituo hicho cha kijeshi, ambacho hapo awali ilikuwa chini ya jukumu la Jeshi la Ulinzi la ATMIS (KDF), kiko katika Jimbo la Jubaland kusini mwa Somalia.
Naibu mwakilishi maalum wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU nchini Somalia Sivuyile Thandikhaya Bam, aliyekabidhi kambi hiyo amesisitiza dhamira ya ATMIS ya kuunga mkono mpango wa mpito wa Somalia kurejesha amani na utulivu katika eneo hilo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma