Vyombo vya habari vya Kenya na China vyasaini makubaliano ya kubadilishana maudhui

(CRI Online) Julai 02, 2024

Watu wakihudhuria hafla ya ufunguzi wa Ukumbi wa Burudani wa China TV huko Nairobi, Kenya, Julai 1, 2024. (Xinhua/Han Xu)

Watu wakihudhuria hafla ya ufunguzi wa Ukumbi wa Burudani wa China TV huko Nairobi, Kenya, Julai 1, 2024. (Xinhua/Han Xu)

Vyombo vya habari vya Kenya na China vimesaini makubaliano ya ushirikiano kuboresha mabadilishano ya maudhui ambayo yanaendeleza maelewano ya kitamaduni ya kuvuka mpaka kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Maofisa wa ngazi ya juu, wakurugenzi wa vyombo vya habari na waundaji wa maudhui walishiriki katika hafla ya ufunguzi wa Ukumbi wa Burudani wa China TV na kusaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya habari na burudani, inayolenga kuboresha mawasiliano kati ya watu wa Kenya na China.

Hafla hiyo iliyofanyika jijini Nairobi, ilifadhiliwa na Idara ya Kitaifa ya Radio na Televisheni ya China (NRTA) na kuandaliwa na kampuni ya StarTimes Kenya.

Watu wakitumbuiza katika hafla ya ufunguzi wa Ukumbi wa Burudani wa China TV huko Nairobi, Kenya, Julai 1, 2024. (Xinhua/Han Xu)

Watu wakitumbuiza katika hafla ya ufunguzi wa Ukumbi wa Burudani wa China TV huko Nairobi, Kenya, Julai 1, 2024. (Xinhua/Han Xu)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha