Watu 39 wauawa katika maandamano ya kupinga muswada wa nyongeza ya kodi nchini Kenya

(CRI Online) Julai 03, 2024

Watu 39 wameuawa na wengine 361 kujeruhiwa katika maandamano ya hivi karibuni ya kupinga nyongeza ya kodi yaliyofanyika nchini Kenya, wakati vijana nchini humo walipoendelea kuingia mtaani jana Jumanne katika raundi mpya ya maandamano hayo.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu (KNHCR) Roseline Odede amesema katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu jioni mjini Nairobi kuwa, takwimu hizo zinajumuisha kipindi cha kuanzia Juni 18 hadi Julai Mosi, na zinaonyesha kuwa jiji la Nairobi linaongoza kwa idadi ya vifo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha