

Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa uratibu ili kupambana na ugaidi barani Afrika
(CRI Online) Julai 03, 2024
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuimarisha uratibu ili kupambana na ugaidi na itikadi zenye mirengo mikali barani Afrika.
Katika ujumbe wake kwa njia ya video kweye Mkutano wa Jukwaa la Amani na Maendeleo Endelevu la Aswam, Guterres amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuunga mkono fursa ya Afrika kama kikapu cha chakula duniani na matamanio yake ya kuwa nguvu kubwa ya nishati ya kijani, huku ikihakikisha kuwa madini muhimu yanawanufaisha Waafrika kwanza.
Amesema jukwaa la Aswan linafanyika wakati Afrika na Dunia iko katika wakati mgumu, kwa kuwa amani na maendeleo vinazuiwa na changamoto kubwa zinazoathiri Afrika na Waafrika kwa kiwango kikubwa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma