Kongamano kubwa la uwekezaji la Afrika Mashariki latazamiwa kufanyika Dar es Salaam na kuvutia wawekezaji wa sekta mbalimbali

(CRI Online) Julai 03, 2024

Kongamano kubwa la wafanyabiashara la Afrika Mashariki “East Africa Investment Forum" linatazamiwa kufanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam na kuvutia wawekezaji wa sekta mbalimbali.

Mwenyekiti wa Chama cha watoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Tanzania (TAFINA), Cynthia Ponera, amesema kongamano hilo kubwa lina lengo la kuunganisha wafanyabisahara hususan watoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, na kwenye kuandaa kongamano hilo, wamepata ushirikiano mkubwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambao pia watashiriki.

Amesema kampuni 62 zinatarajiwa kushiriki, ikiwa ni pamoja na washiriki kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kongamano hilo litasaidia kuwaleta wawekezaji watakaoangalia fursa za uwekezaji nchini Tanzania.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha