Xi asema atajiunga na Tokayev kwa kuhimiza ujenzi wa jumuiya thabiti ya uhai zaidi ya China na Kazakhstan yenye mustakabali wa pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2024

Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev huko Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev huko Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

ASTANA - Rais wa China Xi Jinping kwenye mkutano wake na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev katika ikulu ya Astana siku ya Jumatano amesema kwamba angependa kujiunga na Tokayev katika kujenga pamoja jumuiya ya China na Kazakhstan yenye mustakabali wa pamoja ili iwe jumuiya yenye uhalisia na inayojaa nguvu ya uhai, na kuingiza nguvu za kuhimiza juhudi zaidi kwenye maendeleo na utulivu wa kanda hii na sehemu nyingine.

Katika mazungumzo yao ya kikundi, Rais Xi ameeleza kuwa mwaka jana Tokayev na yeye walikutana mara mbili mjini Xi'an na Beijing mtawalia, na kupanga mipango mipya ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Kazakhstan, kwa kuongoza "miaka 30 ya dhahabu" ya maendeleo ya kasi ya uhusiano kati ya China na Kazakhstan.

Amesema, upande wa China siku zote umekuwa ukitendea uhusiano wake na Kazakhstan kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na kuiwekea mkazo Kazakhstan katika mambo ya diplomasia ya ujirani mwema ya China na kuichukulia kuwa mshirika muhimu wa ushirikiano katika Asia ya Kati.

Rais Xi amesema nia na dhamira ya China ya kudumisha na kukuza uhusiano wa pande mbili ni thabiti, na haitabadilika kutokana na tukio au mabadiliko yoyote katika hali ya kimataifa.

“China daima itakuwa jirani na mshirika mwema ambaye Kazakhstan anaweza kumtegemea na kumwamini,” ameongeza.

Rais Xi pia amesema, upande wa China utaendelea kuimarisha ushirikiano na Kazakhstan katika nishati ya jadi kama vile gesi asilia, kupanua ushirikiano wa nishati mpya ikiwa ni pamoja na umeme unaotokana na nishati ya jua na upepo, kuhimiza kampuni zaidi za China kuwekeza nchini Kazakhstan, na kusaidia Kazakhstan kubadilisha nguvu bora ya rasilimali zake kuwa uwezo wa maendeleo ili kufikia maendeleo ya kijani, na ya kutoa kaboni chache na endelevu.

Kwa upande wake Tokayev amesema ziara hiyo ya Rais Xi nchini Kazakhstan ina umuhimu wa kihistoria kwa maendeleo ya uhusiano wa Kazakhstan na China, akiipongeza China kama jirani rafiki, rafiki wa karibu na wenzi muhimu wa kimkakati wa nchi yake.

“Kwenye msingi imara wa urafiki na ujirani mwema na kuungana mkono kithabiti, uhusiano kati ya Kazakhstan na China umeonyesha mwelekeo wa maendeleo mazuri ambayo haukutokea hapo kabla,” amesema Tokayev, akiongeza kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika ushirikiano kwenye sekta za biashara, nishati, kilimo, na madini, hali ambayo imenufaisha watu wa nchi hizo mbili na kuweka mfano mzuri kwa uhusiano kati ya serikali.

“Kazakhstan ingependa kushirikiana na China katika kutumia fursa zaidi za ushirikiano wa pande mbili katika nishati, madini, nishati mpya na mafungamano ya mawasiliano na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa pande mbili kwenye ngazi mpya,” amesema.

Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev wakikagua gwaride la heshima  huko Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev wakikagua gwaride la heshima huko Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

Rais Xi Jinping wa China akihudhuria akishiriki kwenye hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev  huko Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China akishiriki kwenye hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev huko Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev wakifanya mazungumzo ya kikundi  huko Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev wakifanya mazungumzo ya kikundi huko Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev wakifanya mazungumzo ya watu wengi  huko Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev wakifanya mazungumzo ya watu wengi huko Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev wakitia saini taarifa ya pamoja ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Kazakhstan, na kushuhudia  kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano wa pande mbili katika  sekta za uchumi na biashara,  mafungamano ya mawasiliano , usafiri wa anga na anga ya juu, elimu na vyombo vya habari, baada ya mazungumzo yao mjini Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Ju Peng)

Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev wakitia saini taarifa ya pamoja ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Kazakhstan, na kushuhudia kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano wa pande mbili katika sekta za uchumi na biashara, mafungamano ya mawasiliano, usafiri wa anga na anga ya juu, elimu na vyombo vya habari, baada ya mazungumzo yao mjini Astana, Kazakhstan, Julai 3, 2024. (Xinhua/Ju Peng)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha