Barabara Kuu ya kuvuka bahari kati ya Shenzhen na Chongshan yapitisha magari 305,000 saa 72 baada ya kufunguliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2024

Picha hii iliyopigwa Juni 19, 2024 inaonyesha Barabara Kuu ya Kuunganisha Shenzhen na Zhongshan katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Xinhua/Liu Dawei)

Picha hii iliyopigwa Juni 19, 2024 inaonyesha Barabara Kuu ya Kuunganisha Shenzhen na Zhongshan katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Xinhua/Liu Dawei)

GUANGZHOU – Barabara Kuu kati ya Miji ya Shenzhen na Zhongshan, ambayo ni barabara kuu ya kupita baharini katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, ilikuwa imepitisha magari 305,000 hadi kufikia saa 9 alasiri siku ya Jumatano, saa 72 tu baada ya kufunguliwa rasmi, takwimu kutoka kwa Kampuni ya Usafiri ya Guangdong zimeonyesha.

Ikiwa na urefu wa kilomita 24, barabara hiyo ina madaraja mawili, visiwa viwili vilivyotengenezwa, na handaki la chini ya maji baharini. Inapunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kusafiri kati ya Mji wa Zhongshan na mji kitovu cha teknolojia wa Shenzhen, ambayo iko pande tofauti za Kingo za Mto Pearl katika Mkoa wa Guangdong. Barabara hiyo inapunguza muda wa safari kati ya maeneo hayo mawili kutoka saa mbili hadi dakika takriban 30.

"Barabara hiyo tayari imechukua asilimia takriban 25 ya usafiri wa kila siku wa kupita Mto Pearl, ambayo inakuza mafungamano ya soko katika Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao (GBA)," amesema Lin Feiming, mkuu wa idara ya usafiri ya mkoa huo wa Guangdong.

GBA, inayojumuisha Hong Kong, Macao na miji tisa mkoani Guangdong, inajivunia jumla ya watu zaidi ya milioni 80. Ilipata pato la jumla la kiuchumi la yuan zaidi ya trilioni 14 (karibu dola za Kimarekani trilioni 1.96) Mwaka 2023.

Kabla ya kuzinduliwa kwa barabara hiyo mpya, kulikuwa njia tatu za kuvuka bahari, lakini foleni imekuwa suala kubwa la usafiriwa watu na usafirishaji wa bidhaa katika eneo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha