

Lugha Nyingine
Tume ya SADC yakamilisha operesheni dhidi ya ugaidi kaskazini mwa Msumbiji
Tume ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SAMIM) imetangaza uamuzi wake wa kuondoa vikosi vyake vya kijeshi kutoka Jimbo la Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji, ikiashiria kumalizika kwa jukumu lake la ulinzi wa amani katika jimbo hilo.
Hafla ya kuondoa vikosi hivyo iliongozwa na Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji Cristovao Chume na Mkuu wa SAMIM Mpho Molomo na imefanyika katika mji mkuu wa jimbo hilo la Cabo Delgado, Pemba.
Chume amesema, kambi za magaidi zimeharibiwa na shughuli za kiuchumi zimeanza tena katika jimbo hilo, huku watu waliokimbia makazi yao wakirejea na hali ya usalama kuimarika.
Ameonya kuwa, licha ya mafanikio na kuondoka kwa vikosi vya SAMIM, bado kuna harakati za kigaidi katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo, zikisababisha ukosefu wa usalama kwa wakazi wa maeneo hayo.
Tume ya SADC nchini Msumbiji ilitumwa mwezi Julai, 2021 baada ya kupitishwa na Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Nchi na Serikali za SADC, ikiwa ni mwitikio wa chombo hicho cha kikanda kuunga mkono juhudi za Msumbiji katika kupambana dhidi ya ugaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma