Muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto washinda uchaguzi wa bunge wa Ufaransa, Waziri Mkuu aahidi kujiuzulu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2024

Picha hii iliyopigwa tarehe 28 Juni 2024 ikionyesha Mnara wa Eiffel ukiwa na pete za Olimpiki mjini Paris, Ufaransa. (Xinhua/Sun Fei)

Picha hii iliyopigwa tarehe 28 Juni 2024 ikionyesha Mnara wa Eiffel ukiwa na pete za Olimpiki mjini Paris, Ufaransa. (Xinhua/Sun Fei)

PARIS - Muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto, New Popular Front (NFP), umeshinda duru ya pili ya uchaguzi wa bunge wa Ufaransa, na unatarajiwa kupata viti kati ya 175 na 205 katika Bunge la Ufaransa, kwa mujibu wa makadirio ya hesabu za mwisho za kura yaliyochapishwa na kampuni ya utafiti ya Elabe.

Muungano wa vyama vya siasa unaoongozwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron umepata nafasi ya pili kwa uwezekano wa kupata viti 150 hadi 175, wakati chama cha mrengo mkali wa kulia na vyama washirika wake kwa pamoja vitapata viti 115 hadi 150 pekee, makadirio hayo ya Elabe yanaonesha.

Hakuna chama ambacho kitapata wingi kamili wa viti 289 katika Bunge la Ufaransa lenye wabunge 577.

Akizungumza baada ya kuchapishwa kwa makadirio kadhaa ya kuthibitisha ushindi wa NFP, mkuu wa muungano huo wa vyama vya mrengo wa kushoto wa Ufaransa Jean-Luc Melanchon, "amepongeza" juhudi na uhamasishaji wa watu wa Ufaransa ambao wamepiga kura kuunga mkono NFP.

"Watu wetu wameepuka wazi suluhu mbaya zaidi kwao," amesema, akimaanisha chama cha mrengo mkali wa kulia, National Rally (RN).

"Tumepata matokeo ambayo tuliambiwa hayawezekani," amesema Melanchon, mkuu wa chama cha mrengo wa kushoto La France Insoumise.

Mtu akipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura mjini Paris, Ufaransa, Julai 7, 2024. (Picha na Julien Mattia/Xinhua)

Mtu akipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura mjini Paris, Ufaransa, Julai 7, 2024. (Picha na Julien Mattia/Xinhua)

"Waziri mkuu lazima ajiuzulu. Rais lazima aruhusu New Popular Front kutawala," amesema.

Rais wa zamani wa Ufaransa Francois Hollande, mwanachama wa Chama cha Kisoshalisti cha Ufaransa (PS) na mgombea wa New Popular Front (NFP), amechaguliwa kuwa mbunge vile vile kufuatia duru hiyo ya pili.

Ingawa National Rally imeshindwa kuwa chama kikubwa zaidi katika Bunge la Kitaifa, bado kitakuwa na viti vingi zaidi kuliko bunge lililopita.

Waziri Mkuu wa Ufaransa Gabriel Attal ametangaza Jumapili usiku kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron siku ya Jumatatu, kufuatia kushindwa kwa muungano wa mrengo wa kati wa Macron kwenye uchaguzi huo.

Watu wakipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura huko Clichy-La-Garenne, karibu na Paris, Ufaransa, Julai 7, 2024. (Xinhua/Gao Jing)

Watu wakipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura huko Clichy-La-Garenne, karibu na Paris, Ufaransa, Julai 7, 2024. (Xinhua/Gao Jing)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha