Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Belarus wafanya mazungumzo mjini Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 09, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus Maksim Ryzhenkov mjini Beijing, China, Julai 8, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Belarus Maksim Ryzhenkov mjini Beijing siku ya Jumatatu akisema kuwa China inapenda kushirikiana na Belarus kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili na kuhimiza ushirikiano wa kimkakati wa pande zote na wa hali zote kati ya China na Belarus kuendelea kuimarishwa.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema, China inapenda kuchukua uenyekiti wa zamu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kama fursa ya kushirikiana na pande zote ili kuendeleza moyo wa Shanghai na kujenga nyumba ya pamoja ya SCO katika mshikamano na kuaminiana, amani na utulivu, ustawi na maendeleo, ujirani mwema na urafiki, pamoja na haki na usawa.

Kwa upande wake Ryzhenkov amesema kuwa Belarus inatilia maanani sana uhusiano kati yake na China, na China ni nchi ya kwanza anayoitembelea baada ya kuchukua wadhifa wa waziri wa mambo ya nje.

Ameishukuru China kwa kuiunga mkono Belarus kujiunga na SCO.

“Belarus inathamini sana na itaendelea kushiriki kwa kina katika mfululizo wa mipango ya kimataifa iliyopendekezwa na China, na kufuata utaratibu wa ushirikiano wa pande nyingi kushughulikia kwa pamoja changamoto za kimataifa,” Ryzhenkov amesema.

Pande hizo mbili pia zimebadilishana maoni kuhusu mgogoro wa Ukraine ambapo Ryzhenkov amezungumzia sana juu ya makubaliano ya pointi sita yaliyotolewa kwa pamoja na China na Brazil.

Wang amesema kipaumbele cha kwanza ni kufuata kanuni tatu za kutopanua uwanja wa vita, kutochochea mapigano, na kutowasha moto kwa upande wowote, ili kutuliza na kupoza mgogoro huo na kuweka mazingira ya kuanzisha upya mazungumzo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus Maksim Ryzhenkov mjini Beijing, China, Julai 8, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus Maksim Ryzhenkov mjini Beijing, China, Julai 8, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha