Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ahimiza kuchukulia hatua za haraka kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 09, 2024

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed akihutubia mkutano wa ufunguzi wa Baraza la Kisiasa la Ngazi ya Juu Mwaka 2024 kuhusu Maendeleo Endelevu (HLPF) kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Julai 8, 2024. (Loey Felipe/Picha ya UN/ Xinhua)

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed akihutubia mkutano wa ufunguzi wa Baraza la Kisiasa la Ngazi ya Juu Mwaka 2024 kuhusu Maendeleo Endelevu (HLPF) kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Julai 8, 2024. (Loey Felipe/Picha ya UN/ Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed siku ya Jumatatu ametaka dhamira ya mara moja kwa sera thabiti na suluhu lenye uvumbuzi ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ifikapo Mwaka 2030.

Akizungumza kwenye Baraza la Kisiasa la Ngazi ya Juu Mwaka 2024 kuhusu Maendeleo Endelevu (HLPF), Mohammed amesisitiza haja ya haraka ya kuchukua "hatua za kimageuzi" ili kukabiliana na changamoto kubwa za kimataifa kama vile umaskini, ukosefu wa chakula na mabadiliko ya tabianchi.

"Ingawa changamoto kubwa zilizo mbele yetu ni za kutisha, kwa pamoja tunaweza kuzishinda, kufikia mustakabali wenye amani, ustawi na endelevu ambao watu wote siyo tu wanauhitaji bali wanaustahili," amewaambia wajumbe wanaohudhuria baraza hilo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Akirejelea juu ya njia ya kutimiza Ajenda ya 2030, Mohammed amesisitiza umuhimu wa Mkutano ujao wa Kilele wa Siku za Baadaye. "Mkutano huo ni fursa nzuri ya kurekebisha imani iliyomomonyoka na kuonyesha kwamba ushirikiano wa kimataifa -- binadamu wakishikamana kukabiliana na fursa na vitisho -- vinaweza kutupeleka mbele," amesema.

Mohammed amezungumzia changamoto mbalimbali za jumuiya ya kimataifa, kutoka kwa umaskini hadi mabadiliko ya tabianchi, na ukweli wa kusikitisha kwamba chini ya moja ya tano ya malengo ya SDGs yako hatarini.

"Lakini pia inarekebishika ... hii ndiyo umuhimu wa Baraza hili -- kutafuta suluhu na dhamira ya kisiasa kubadilisha maneno yetu kuwa vitendo katika maisha ya watu katika mabilioni," amebainisha, akiimarisha uwezo wa pamoja wa kushinda changamoto hizi na kufikia mustakabali endelevu wa siku za baadaye kwa wote.

Baraza hilo, ambalo linafanyika kuanzia Julai 8 hadi Julai 17, likilenga kutathmini maendeleo kuelekea malengo kadhaa ya maendeleo endelevu, yakiwemo yale ya yanayolenga kutokomeza umaskini, njaa kali, hatua za tabianchi, jamii zenye amani na ujumuishaji, na kuimarisha mbinu za utekelezaji.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha