Wataalamu waitaka EAC kukubali Kiswahili kuwa lugha rasmi ya kikanda

(CRI Online) Julai 09, 2024

Wataalamu wamerejea tena mwito kwa baraza la mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuharakisha marekebisho ya Mkataba wa EAC kuiwezesha lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya kanda hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na makao makuu ya Jumuiya ya EAC huko Arusha, wataalamu hao wamezitaka nchi zote wanachama kutunga sheria ya kuhimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli iliyofanyika huko Mombasa.

Waziri wa jinsia, utamaduni, sanaa na urithi wa Kenya Bi. Aisha Jumwa amesema, Kiswahili ni lugha ya umoja katika kanda hiyo, inayotumiwa na watu zaidi ya milioni 200. Amehimiza nchi zote wanachama wa EAC kuhimiza sheria na sera ziandikwe na kuchapishwa kwa lugha ya Kiswahili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha