DRC yaendelea na juhudi za kidiplomasia wakati kukiwa na makubaliano na kundi la M23

(CRI Online) Julai 09, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Bw. Therese Kayikwamba Wagner amesema DRC itashiriki katika juhudi za kidiplomasia wakati na baada ya usimamishaji vita wa kibinadamu na kundi la M23, ambalo limetwaa sehemu kubwa ya mashariki mwa nchi hiyo.

Usimamishaji vita huo wa siku 14, kuanzia Julai 5 hadi 19, unajumuisha dira ya utekelezaji iliyowekwa kwa ajili ya kurejea kwa amani mashariki mwa nchi hiyo.

Waziri huyo amesema usimamishaji huo vita haumaanishi kuwa serikali inaacha kuwa macho, akisema juhudi za kidiplomasia zinalenga "suluhisho la kudumu" la kurejesha amani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha