Kutembea pamoja kwenye njia pana | China na Kazakhstan zashirikiana kuwasha mwanga wa mafungamano ya ustaarabu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 10, 2024

Kazakhstan, nchi yenye mbuga pana, ni kituo muhimu ambacho ustaarabu wa Mashariki na Magharibi unakutana. Nchi hii ndipo Njia ya Kale ya Hariri ilipopita.

Hivi karibuni, timu ya mahojiano ya “Njia ya Hariri ya Utamaduni” ya wanahabari wa People’s Daily Online ilikwenda Kazakhstan, wakijionea kiwango cha juu cha mabadilishano kati ya China na Kazakhstan katika sekta mbalimbali na kutafuta njia ya ustaarabu tofauti kuishi pamoja kwa mapatano.

Mahali ambapo kwa mara ya kwanza pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lilipendekezwa

Tarehe 7, Septemba, 2013, Rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba nchini Kazakhstan na kupendekeza kwa mara ya kwanza pendekezo la kujenga pamoja “Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri.”

Katika muongo uliopta, ushirikiano wa kimataifa wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umestawi na kupata matunda mbalimbali.

Hadi 2023, kiwango cha biashara kati ya China na Kazakhstan kilizidi kwa mara ya kwanza dola za Marekani bilioni 40, kikifikia dola za Marekani bilioni 41 na kuongezeka kwa asilimia 32 kuliko mwaka uliotangulia.

Nembo ya simu janja “Xiaomi” inayovutia kutazama kwenye maduka ya bidhaa za kielektroniki, chapa nyingi za magari ya China kama vile Geely, Chery na BYD yanayokimbia barabarani......Vyote hivyo ni ushahidi wa biashara kati ya China na Kazakhstan yenye ustawi.

Mpaka mwezi Machi, 2024, China na Kazakhstan zilikuwa zimeanzisha uhusiano wa kirafiki kati ya jozi 26 za mikoa (majimbo) na miji. Watu wa nchi hizo mbili wanawasiliana mara kwa mara, na urafiki ambao umerithishwa kwa maelfu ya miaka umekita zaidi mizizi mioyoni mwa watu.

Urafiki uliorithishwa Kizazi hadi Kizazi

Katika mji wa kale wa Almaty kwenye Njia ya Hariri, kuna barabara ya Xian Xinghai (Mwanamuziki maarufu na mtunzi wa zamani wa nyimbo wa China). Mnara wa kumbukumbu ya Xian Xinghai unasimama kimya kimya hapa, ukikumbuka simulizi inayogusa moyo.

Mnamo mwaka 1941, Xian alikwenda Almaty. Wakati Xian aliposumbuliwa na umaskini na maradhi, mwanamuziki wa Kazakhstan Bakhitzhan Baykadamov alimpa makazi kwa wema. Akiwa huko Xian alikamilisha shairi lake maarufu la “Muziki wa Mto Manjano (Yellow River Concerto)”, na pia alitunga wimbo la kumsifu shujaa wa Kazakhstan “Amangeldy”, ambalo lilikaribishwa sana na watu wa nchi hiyo.

Mwaka 2019, filamu iliyotengenezwa kwa pamoja na pande za China na Kazakhstan “Mwanamuziki” ilitolewa rasmi, ikileta simulizi hiyo ya kugusa kwenye skrini ya sinema.

Wakati wa miaka ya vita, familia ya Bakhitzhan Baykadamov na Xian Xinghai walijenga urafiki wa kweli wakati wa dhiki. Methali ya Kazakhstan inasema: “Kama ukiokoa maisha ya mtu, kondoo wako atazaa mapacha.” Hii inaendana na utamaduni wa jadi wa China wa kusaidiana katika dhiki na kuwapenda wengine.

Kwenye Kituo cha Tiba ya Jadi cha China-Kazakhstan kilichoko Astana, mji mkuu wa Kazakhstan, “wema” wa madaktari unawasilishwa kupitia matibabu makini ya tiba ya jadi ya China.

Baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa, kupitia simulizi za miongoni mwa wagonjwa wengine, Gulzhina alikuja kwenye kituo hicho kupokea matibabu ya kurejea kwenye hali ya afya. Matibabu hayo yaliboresha uwezo wake wa kutembea. Wakati wa muda mfupi wa kusubiria matibabu, aliuliza kwa hamu ni lini kituo kitapanuliwa na lini matibabu mapya ya dawa za jadi za China yataanzishwa.

Tangu kilipozinduliwa Desemba, 2022, kituo hicho kimepokea wagonjwa karibu 8,000, na kufanya mkutano wa mashauriano ya kimataifa zaidi ya 200 kupitia video.

Kufunzana na kunufaishana kwawasha mwanga wa mafungamano ya ustaarabu wa binadamu

Wakazakh wana usemi wa jadi wa: “Nyimbo na farasi ni mabawa mawili ya Wakazakh.” Watu wanapokuja Kazakhstan watapata kutambua kuwa, utamaduni wa muziki na farasi pia ni madaraja ya mafungamano na kufunzana kati ustaarabu tofauti.

Kwenye Jumba la Makumbusho la Ala za Muziki la Almaty, ala za muziki za kijadi za makabila ya watu wa Asia ya Kati Dombra, Gitaa la Ulaya, ala za muziki za China Erhu, na ala za muziki kutoka maeneo mengine zimewekwa na kuoneshwa kwa pamoja.

Kwa maoni ya msomi wa utamaduni wa China kutoka Kazakhstan Clara Hafizova, uhusiano wa karibu kati ya farasi na mashujaa umeoneshwa kwa udhahiri kwenye riwaya ya kale ya China “Madola Matatu” (Romance of the Three Kingdoms), hali ambayo inafanana na simulizi ya mashujaa na farasi katika historia ya Kazakhstan.

Hivi leo, mabadilishano ya kitamaduni kati ya China na Kazakhstan yanajionesha kwa namna nyingi zaidi.

Kwenye duka la vitabu la Almaty vitabu zaidi ya 1,000 vya maudhui mbalimbali ya siasa, historia na utamaduni wa China na kadhalika vimepangwa vizuri. Mhusika wa duka hilo Zhanar Kazhimova amejulisha kuwa, kutokana na kuongezeka kwa “wimbi la lugha ya Kichina”, biashara ya duka hilo imestawi siku hadi siku.

Kuanzia mafungamano ya ustaarabu katika njia ya hariri ya kale, hadi kuchangia katika vita dhidi ya Ufashisti, hadi hivi leo pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kuanzia hapa na kwenda duniani kote, China na Kazakhstan, kama majirani wazuri, washirika wazuri na ndugu wazuri, bila shaka zitafanya kazi bega kwa bega kuendelea kutunga sura mpya na nzuri ya urafiki kati ya nchi hizo mbili wa kizazi hadi kizazi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha