Xi Jinping atoa amri ya kumpandisha cheo ofisa wa kijeshi hadi kuwa na cheo cha jenerali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 10, 2024

Xi Jinping, Rais wa China, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa cheti cha amri ya kumpandisha cheo naibu mkurugenzi mtendaji wa  Ofisi ya Kazi ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya Kijeshi   He Hongjun, hadi kuwa na cheo cha jenerali kwenye hafla iliyofanyika kwa ajili ya upandishaji cheo mjini Beijing, China, Julai 9, 2024. (Xinhua/Li Gang)

BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), siku ya Jumanne alitoa cheti cha amri ya kumpandisha cheo ofisa wa kijeshi hadi kuwa na cheo cha jenerali, ambacho ni cheo cha juu zaidi cha maofisa wa kijeshi walio katika utumishi nchini China, ambapo aliyepandishwa cheo hicho ni ofisa He Hongjun, naibu mkurugenzi mtendaji wa Ofisi ya Kazi ya Kisiasa ya CMC.

Zhang Youxia, naibu mwenyekiti wa CMC, alitangaza amri hiyo, ambayo imetiwa saini na Rais Xi katika hafla iliyofanyika kwa ajili ya upandishaji huo wa cheo mjini Beijing. He Weidong, ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa CMC, aliongoza hafla hiyo.

Rais Xi ametoa pongezi kwa ofisa huyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha