China ingependa kushirikiana na Afrika kwa kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa: Naibu Waziri Mkuu wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 10, 2024

Naibu Waziri Mkuu wa China Liu Guozhong, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Rukia Nakadama, naibu waziri mkuu wa tatu wa Uganda, ambaye anahudhuria Mkutano wa 5 wa Baraza la Ushirikiano wa Serikali za Mitaa kati ya China na Afrika, Julai 9, 2024. (Xinhua/Chen Yehua)

GUANGZHOU - China ingependa kutoa fursa mpya kwa Afrika kuhusu maendeleo yake na kuungana mkono katika kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa, Naibu Waziri Mkuu wa China Liu Guozhong amesema siku ya Jumanne huko Guangzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China wakati akihutubia hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 5 wa Baraza la Ushirikiano wa Serikali za Mitaa kati ya China na Afrika.

Liu, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema China na Afrika zimefanya kazi pamoja katika kuzidisha na kuimarisha uhusiano na pande hizo mbili zimeingia katika hatua mpya ya kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na Afrika ya kiwango cha juu yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

Akieleza kuwa Dunia sasa ni yenye hali ya utatanishi na misukosuko, huku mabadiliko ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita yakiongezeka kwa kasi, Liu amesema China na Afrika zinahitaji kuimarisha mshikamano na ushirikiano zaidi kuliko wakati wowote wa hapo kabla.

Liu amesema serikali za mitaa za China na Afrika zinapaswa kutendeana kwa usawa na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja, na kupanua nyanja za ufunguaji mlango na ushirikiano.

Liu akisisitiza kufanya uvumbuzi na ametoa wito kwa pande zote mbili kuharakisha wa kubadilisha miundo ya uzalishaji iwe ya kijani, huku zikishikilia ujumuishaji na kufundishana, na kuhimiza mawasiliano katika mambo ya utamaduni.

“China ingependa kuhimiza muunganisho kati ya ujenzi wa pamoja wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia, Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia, Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika na mikakati ya maendeleo ya nchi za Afrika,” Liu ameongeza.

Viongozi takriban 350 wa kisiasa kutoka nchi za Afrika na maofisa wa serikali za mitaa na taasisi husika kutoka China na Afrika wamehudhuria mkutano wa baraza hilo. 

Naibu Waziri Mkuu wa China Liu Guozhong, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akihutubia hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 5 wa Baraza la Ushirikiano wa Serikali za Mitaa kati ya China na Afrika, mjini Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Julai 9, 2024. (Xinhua/Chen Yehua)

Naibu Waziri Mkuu wa China Liu Guozhong, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Christian Ntsay, waziri mkuu wa Madagascar, ambaye anahudhuria Mkutano wa 5 wa Baraza la Ushirikiano wa Serikali za Mitaa kati ya China na Afrika, Julai 9, 2024. (Xinhua/Chen Yehua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha