Zimbabwe yatafuta kuimarisha ushirikiano na China kwenye sekta ya sanaa

(CRI Online) Julai 10, 2024

Mkurugenzi wa Baraza la Sanaa Taifa la Zimbabwe (NACZ), Napoleon Nyanhi amesema, Zimbabwe inatafuta kuimarisha ushirikiano na China kwenye sekta ya sanaa za ubunifu ili kukuza sekta hiyo na kuhimiza uhusiano wa kiutamaduni kati ya pande hizo mbili.

Akihojiwa na shirika la habari la China, Xinhua pembezoni mwa Jukwaa la kwanza la Harare kuhusu Wiki ya Afrika na Taaluma, Bw. Nyanhi amesema mabadilishano mengi yamefanyika kwenye sanaa za maonesho, kama vile muziki, ngoma na upigaji wa ala na kwamba Zimbabwe inatarajia ushirikiano zaidi na China kwenye maeneo mengine ya sanaa, ikiwemo ubunifu wa mitindo, uandaaji wa filamu na vipindi vya televisheni.

Bw. Nyanhi pia amelitaja shindano la Dreamstar lililofadhiliwa na China, ambalo ni shindano kubwa zaidi la aina yake la kutafuta vijana wenye vipaji nchini Zimbabwe, akisema kuwa lina umuhimu mkubwa katika kuhamasisha wasanii wa fani mbalimbali nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha