Moody's yashusha makadirio ya uwezo wa Kenya kulipa madeni baada ya serikali kuachana na mswada wa kodi

(CRI Online) Julai 10, 2024

Kampuni ya kimataifa la Ukadiriaji wa Mambo ya Fedha, Moody's limeshusha makadirio ya uwezo wa Kenya kulipa mikopo, ikirejelea "kukosekana kwa uwezo wa kutekeleza hatua za kubana matumizi kutokana na kuondolewa bungeni kwa Muswada wa Fedha wa Mwaka 2024.

Moody’s pia imeshusha daraja la Kenya katika ukadiriaji wa wajibu wa muda mrefu wa madeni ya fedha za kigeni na za nje hadi "Caa1" kutoka "B3".

Taarifa hiyo imetolewa baada ya Rais William Ruto wa Kenya kulazimika kuondoa bungeni Mswada wa Fedha wa 2024 ambao ulikuwa na mpango mpya wa utozaji kodi kufuatia wiki tatu za maandamano ya umma.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha