

Lugha Nyingine
Kenya yahimiza ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi ili kuimarisha utalii wa matembezi
(CRI Online) Julai 10, 2024
Bodi ya Utalii ya Kenya (KTB) imesema inatumia ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ili kuchochea fursa za utalii unaohusisha matembezi binafsi na kujionea mambo mapya ya kiikolojia na mazingira (adventure) nchini Kenya.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa KTB Bibi June Chepkemei amesema utalii wa namna huyo umeonesha uthabiti na uwezo wa kukaribisha watalii zaidi nchini Kenya. Utalii huo licha ya kuwa endelevu pia una uwezo wa kuunga mkono uchumi wa wenyeji.
Ametaja uzoefu anuwai wa utalii wa aina hiyo kuwa ni pamoja na kutazama wanyama kwa njia rafiki kwa mazingira, kuwatazama ndege, kupanda milima na michezo ya kwenye maji.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma