

Lugha Nyingine
Rais Kagame asema Rwanda inataka kudumisha uhusiano imara na China
(CRI Online) Julai 15, 2024
Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema kwamba Rwanda ina uhusiano imara na China, na inataka kudumisha uhusiano huo.
Kagame ameyasema hayo siku ya Jumamosi kwenye mkutano na wanahabari mjini Kigali muda mfupi baada ya kuhitimisha mikutano ya kampeni yake kabla ya uchaguzi wa rais na wabunge utakaofanyika leo Jumatatu.
Kagame alipojibu swali kuhusu uhusiano kati ya Rwanda na China katika miaka 50 iliyopita amesema, Rwanda ina uhusiano mzuri na China, na inataka kudumisha uhusiano huo.
Amesema tofauti na washirika wengine, China inazichukulia Rwanda na nchi nyingine za Afrika kwa kuheshimiana, na haiingilii mambo ambayo inafikiria kuwa ni sahihi kwao.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma