DRC yapongeza kituo cha kuzalisha umeme kwa maji kilichojengwa na China

(CRI Online) Julai 15, 2024

Alexis Gisaro Muvuni (katikati), Waziri wa Nchi anayeshughulikia Miundombinu na Kazi za Ujenzi wa Umma wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akitembelea Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Maji cha Busanga katika Jimbo la Lualaba, DRC, Julai 11, 2024. (Xinhua/Shi Yu)

Waziri wa Nchi anayeshughulikia Miundombinu na Kazi za Ujenzi wa Umma wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Bw. Alexis Gisaro Muvuni, amesema anafurahishwa na mbinu zinazotumiwa katika uendeshaji wa kituo cha kuzalisha umeme kwa maji cha Busanga katika Jimbo la Luabala kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Bw. Muvuni amesema DRC na China zinapaswa kuhimiza uwekezaji katika uzalishaji wa umeme na miundombinu, na kuibua uwezekano katika ushirikiano kwenye uzalishaji wa umeme kwa maji na nishati ya jua.

Mwezi Oktoba 2023, Rais Felix Tshisekedi wa DRC alizindua kituo hicho na kuanzisha uzalishaji wa umeme kwa maji katika kituo hicho. Kituo hicho kimewekezwa na kujengwa kwa pamoja na kampuni za China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha