EAC yasema Uganda itaendesha kongamano la 11 la usimamizi wa mtandao wa intaneti wa Afrika Mashariki

(CRI Online) Julai 16, 2024

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imetoa taarifa siku ya Jumatatu mjini Arusha nchini Tanzania ikisema Uganda itaendesha kongamano la 11 la usimamizi wa mtandao wa intaneti la Afrika Mashariki (EAIGF), ili kutatua masuala makuu ambayo yataongeza maendeleo na usimamizi wa mtandao wa intaneti kwenye kanda hiyo.

Taarifa hiyo imesema EAC ikishirikiana na Jumuiya ya Mtandao wa Intaneti tawi la Uganda, wataendesha kongamano la “Kujenga Mustakabali wa Wadau mbalimbali wa Kidigitali wa Afrika Mashariki” mjini Kampala kuanzia tarehe 11 hadi 12 Septemba.

Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia sekta za miundombinu, uzalishaji, jamii na siasa Andrea Aguer Ariik Malueth ametoa wito kwa wahusika wa sekta ya TEHAMA na wadau wengine kutumia kongamano hilo ili kuweka ajenda ya mafungamano ya kidigitali kwa ajili ya kanda hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha