

Lugha Nyingine
Tanzania yatarajia mtaji wa uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 10 katika mwaka 2024
Kituo cha Uwekezaji nchini Tanzania (TIC) kimesema kimeweka lengo la kuvutia mtaji wa uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani karibu bilioni 10 katika mwaka 2024.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana Jumanne, TIC imesema lengo hilo linatokana na miaka mitano ya ukuaji mkubwa wa uwekezaji wa ndani na wa kigeni unaochochewa na sheria nzuri pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, TIC imesajili miradi 707 ya uwekezaji yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 6.56 wakati serikali ilipofunga mwaka wa fedha wa 2023/2024 Juni 30 mwaka huu, ikiwa ni kiasi cha juu zaidi katika miaka mitano ya fedha iliyopita.
Taarifa hiyo pia imesema, ushiriki wa wazawa pia umeongezeka, huku asilimia 38.19 ya miradi iliyosajiliwa ikimilikiwa na Watanzania, asilimia 42.86 ikimilikiwa na raia wa kigeni, na asilimia 19.38 ikiwa ni ubia kati ya raia wa Tanzania na wa kigeni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma