Lugha Nyingine
Matunda yenye uzito wa tani zaidi ya 50 yagawiwa bila malipo kwa watu huko Mangshi, Yunnan, China
Mji huu mdogo katika Mkoa wa Yunnan wa China unagawa matunda kwa watu bila malipo tena! Siku za hivi karibuni, kwenye Shughuli ya 7 ya Kugawana Matunda ya Kistaarabu na pia Tamasha la Kwanza la Utamaduni wa Watu wa Mji wa Mangshi katika eneo linalojiendesha la Makabila ya Wadai na Wajingpo la Dehong, serikali ya huko iligawa bila malipo kwa wenyeji na watalii matunda yenye uzito wa tani zaidi ya 50 yaliyovunwa kutoka kwenye miti iliyopandwa mitaani.
Wenyeji na watalii wakiwa wamefika kupata matunda katika Shughuli ya 7 ya Kugawana Matunda ya Kistaarabu. (Mpiga picha:Yang Bangqing)
Wenyeji na watalii wakipiga picha pamoja na matunda waliyopata katika Shughuli ya 7 ya Kugawana Matunda ya Kistaarabu. (Mpiga picha:Yang Bangqing)
Mji wa Mangshi unajulikana kwa jina la“Mji wa Maua na Matunda”. Barabara 23 za eneo la mjini zimepandwa kwa pande zake zote mbili na miti ya mifenesi, longan, maembe, mizabibu na miti mingine mingi ya matunda, na kuunda mandhari ya kitropiki ya mji yenye ladha kali za kikabila.
Marundo ya matunda yakiwa kwenye uwanja wa Mangshi na kufanya hali ya hewa kujaa harufu ya matunda.Mpiga picha:Yang Bangqing)
Shughuli ya kugawana Matunda ya Mangshi imekuwa ikifanyika kwa uendelevu kwa miaka mingi. Kila Julai na Agosti ya kila mwaka, serikali ya huko huchuma matunda yaliyoiva katika ukanda wa kijani na kuyagawa kwa watu wenyeji na watalii bila malipo, na kutoa huduma kwa watu wa makundi maalum na wasiojiweza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma