

Lugha Nyingine
Shirika la ndege la Uganda latangaza kuzindua njia tatu mpya za anga barani Afrika
Shirika la ndege la Uganda limetangaza kuzindua njia tatu mpya za safari ya anga zitakazoelekea miji mikuu ya Zambia, Zimbabwe na Nigeria mwezi Septemba mwaka huu wa 2024.
Kwenye hafla ya uzinduzi iliyofanyika Jumatano mjini Kampala, mji mkuu wa Uganda, afisa mtendaji mkuu wa Shirika la Ndege la Uganda, Jenifer Bamuturaki amesema kuwa njia hizo mpya za safari ya anga zitaiunganisha zaidi Uganda na maeneo mengine ya Afrika.
Amesema, kuzinduliwa kwa njia hizo mpya za safari ya anga ni hatua muhimu katika kutoa mchango endelevu kwa safari za ndani ya Afrika. Pia ameeleza kuwa njia hizo za safari za Magharibi na Kusini mwa Afrika zitaleta urahisi kwa wasafiri katika bara zima, na kuleta fursa nyingi katika biashara, utalii, na uhusiano wa kijamii na kitamaduni.
Shirika hilo tayari lina njia za safari katika nchi za Kenya, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Somalia, Sudan Kusini, Afrika Kusini, Umoja wa Falme za Kiarabu, India, Burundi na mji wa Lagos wa Nigeria.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma