Afisa wa Zambia aipongeza China kwa mpango wa mafunzo ya utawala bora

(CRI Online) Julai 18, 2024

Waziri wa Jimbo la Copperbelt nchini Zambia, Elisha Matambo ameipongeza China siku ya Jumatano kwa kutoa mafunzo ya kina katika kujenga uwezo wa utawala bora na mipango ya uchumi mkuu kwa maafisa waandamizi wa serikali ya Zambia.

Matambo, ambaye alikuwa miongoni mwa mawaziri na makatibu wakuu waliopata mafunzo hayo hivi karibuni nchini China, ametoa shukrani kwa serikali ya China kwa kuandaa mpango huo.

Amesema viongozi hao watatumia elimu kubwa waliyopata wakati wa mafunzo hayo ili kuboresha utoaji huduma katika idara mbalimbali za serikali kuu na majimbo.

Aidha amesema viongozi hao walipewa fursa ya kupata uzoefu wa moja kwa moja kwa kutembelea mashirika mbalimbali ya China kama Huawei na PowerChina ili kuelewa zaidi shughuli zao.

Amesisitiza kuwa Zambia inapenda kushirikiana na serikali ya China na kujifunza kutokana na uzoefu wake ili kuboresha maisha ya watu wake.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha