Waangalizi wa kimataifa waipongeza Rwanda kwa mchakato wa uchaguzi wa amani na makini

(CRI Online) Julai 18, 2024

Waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi wameipongeza Rwanda kwa kudumisha "mazingira ya amani ya uchaguzi" na usimamizi makini wakati wa uchaguzi mkuu uliomalizika hivi majuzi.

Katika taarifa ya pamoja siku ya Jumatano iliyosomwa kwenye mkutano na wanahabari mjini Kigali nchini Rwanda, waangalizi hao wanaowakilisha mashirika kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Umoja wa Afrika (AU), Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati, wamepongeza mchakato mzima wa uchaguzi.

Taarifa hiyo imesema pia wametambua kazi yenye bidii ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda (NEC) na taasisi nyingine zinazohusika kusimamia mchakato wa uchaguzi kwa mujibu wa kalenda ya uchaguzi, kwamba uchaguzi umefanyika katika hali ya utulivu na amani iliyowawezesha wagombea kufanya kampeni kwa uhuru.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha