Umoja wa Afrika wapitisha mkakati wa AI na makubaliano ya kidigitali ili kuhimiza maendeleo ya bara la Afrika

(CRI Online) Julai 22, 2024

Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulika na miundombinu, nishati na utandawazi wa kidigitali Bi. Amani Abou-Zeid amesema, kamati ya utendaji imepitisha mkakati wa Akili Mnemba (AI) na makubaliano ya kidigitali ili kuhimiza maendeleo ya kidigitali barani humo.

Akizungumza kwenye mkutano wa kamati ya utendaji ya Umoja wa Afrika uliofanyika Ijumaa huko Accra, mji mkuu wa Ghana, Bi.Abou-Zeid amesema mikakati hiyo itatoa mwelekeo kwa matumizi ya teknolojia ili kutafuta suluhisho la changamoto za Afrika, kusaidia kuharakisha ufuatiliaji wa miradi na mipango mingi, na vilevile kuzuia matumizi yasiyo ya kimaadili ya teknolojia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha